Skip to content
Mwongozo wa Kilimo cha Kahawa | miche.co.tz – Njombe, Tanzania Jiunge na Wakulima wa Kahawa
Kilimo Biashara na miche.co.tz

Kanuni za Kilimo cha Kahawa Kisasa

Jifunze uchaguzi wa miche bora inayozaa sana na kuhimili magonjwa, ratiba ya mbolea kuongeza matunda, na jinsi ya kulinda shamba lako dhidi ya magonjwa hatari ya ukungu na kutu ya majani.

Soma Kanuni Weka Oda Sasa
Aina za Miche
Arabica na Robusta (Compact).
Nafasi Sahihi
Inategemea kama ni Tall au Compact.
Mbolea Muhimu
Fosforasi wakati wa kupanda miche.
Ulinzi wa Zao
Kudhibiti CBD na CLR.

1. Utangulizi

Kahawa ni miongoni mwa mazao makuu ya biashara yanayoingiza fedha nyingi za kigeni nchini Tanzania. Kilimo hiki ni cha muda mrefu (zao la kudumu) ambapo uwekezaji makini katika miche na usimamizi wa shamba unahakikisha mkulima anavuna kwa miongo kadhaa.

Kwa ujumla, kuna aina mbili kuu za kahawa zinazolimwa Tanzania: Arabica (inayostawi kwenye miinuko yenye baridi kali kama Kilimanjaro, Mbeya, Ruvuma, na Songwe) na Robusta (inayostawi kwenye miinuko ya chini na joto kama Kagera na maeneo ya maziwa makuu).

2. Aina za Mbegu na Miche ya Kahawa

Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) imeendelea kuboresha miche ili kuleta aina zenye mavuno mengi na zinazokinzana na magonjwa. Aina zilizopo sokoni zimegawanywa katika makundi haya:

A) Kahawa ya Arabica:

  • Arabica Fupi (Compact Arabica): Hizi ni aina mpya zilizoboreshwa. Zina maumbo mafupi, zinazaa sana, na kubwa zaidi ni kwamba zinakinzana na magonjwa hatari ya chule/kutu ya majani (CLR) na ugonjwa wa buni (CBD). Hupandwa kwa nafasi ya mita 2 x 2.
  • Arabica Ndefu (Tall Arabica): Hizi ni aina za zamani kama vile N39, KP423, na Bourbon. Licha ya kuwa na ladha nzuri sana (premium cup quality), zinashambuliwa sana na magonjwa hivyo zinahitaji gharama kubwa za dawa. Hupandwa kwa mita 2.5 x 2.5 au 3 x 3.

B) Kahawa ya Robusta:

  • Maruku 1 & Maruku 2: Zina uvumilivu mkubwa wa magonjwa hasa mnyauko wa fusarium (CWD). Inazaa sana na kuvumilia ukame kiasi ukilinganisha na aina za asili.

3. Ratiba ya Matumizi ya Mbolea

Ili mti wa kahawa uwe na nguvu ya kubeba matunda mengi kila msimu, unahitaji kupatiwa chakula sahihi kulingana na hatua yake:

Hatua ya Ukuaji / Msimu Aina ya Mbolea / Virutubisho Kazi Yake Kubwa
1. Kuandaa Shimo & Kupanda Samadi / Mboji + Mbolea ya Fosforasi (Mf. DAP, Minjingu) Changanya udongo wa juu na ndoo moja ya samadi pamoja na gramu 100 za DAP. Inasaidia mche kushika mizizi kwa haraka sana (Root establishment).
2. Kipindi cha Ukuaji (Mvua za kwanza) Mbolea za Naitrojeni (CAN, UREA au NPK) Husaidia mti kutoa matawi mapya na majani mengi ya kijani ambayo ndio yatabeba maua msimu unaofuata. Weka gramu 100 mpaka 200 kwa mti kulingana na umri.
3. Kabla na Wakati wa Kutoa Maua Foliar yenye Zinc, Boron Kutoka: Verno + Kinara Faida CalMaBo Zinc na Boron zinasaidia maua kuchanua vizuri na kuepusha maua na vitunda vichanga (pinheads) kudondoka. Booster inaongeza afya ya mmea na kulisha maua.
4. Wakati wa Kujaza Matunda (Berries) Mbolea yenye Potassium (K) nyingi Na Mbolea ya majaniu: Booster Power Jelly Potassium inahusika na kujaza punje za kahawa kuwa na uzito mkubwa (density) badala ya kuwa makapi, na kuboresha ubora (cup quality).
Kudhibiti Tindikali ya Udongo (Soil pH)

Kahawa hustawi kwenye udongo wenye pH ya 5.5 hadi 6.5. Kama udongo wako una asidi nyingi sana (tindikali), inashauriwa kuweka chokaa ya kilimo (Agricultural Lime) miezi miwili kabla ya kuweka mbolea za chumvichumvi ili kuruhusu mti kufyonza virutubisho.

4. Magonjwa na Wadudu wa Kahawa

Kulinda shamba lako ni muhimu ili kuepuka hasara kubwa ya mavuno:

  • Ugonjwa wa Chule (Coffee Berry Disease – CBD): Hushambulia matunda machanga na kufanya yawe meusi na kudondoka au kukauka yakiwa mtini. Tumia dawa za ukungu (Fungicides) kama Copper (Red Copper: Mfano Nordox 75WG) mapema kabla ya mvua. Matumizi ya miche ya Compact huzuia ugonjwa huu.
  • Kutu ya Majani (Coffee Leaf Rust – CLR): Huacha madoa ya njano/machungwa kwa chini ya majani na kufanya majani yadondoke na mti kubaki mtupu. Kinga kwa kupiga dawa za ukungu na kupunguza kivuli kingi shambani Tumia Nordox 75WG.
  • Kimamba (Antestia Bug): Ndio adui mkubwa sana wa kahawa wa kundi la wadudu. Hufyonza maji kwenye matunda na maua na kufanya matunda kuoza, na kupunguza ladha ya kahawa (potato taste). Dhibiti kwa kupiga viuatilifu (Insecticides) vyenye ubora.
  • Borer (Funza wa Shina/Matawi): Hutoboa shina au matawi. Kata matawi yaliyoathirika na kuyachoma, na dhibiti kwa kupiga dawa.
Huduma Zetu kwa Zao Hili
Miche Bora Iliyoboreshwa

Tunatoa ushauri wa wapi kupata miche ya Compact inayozaa haraka na isiyohitaji dawa nyingi za ukungu.

Kinara Faida + Pluto + Booster Power Jelly

Mbolea Za majani (Foliar) zenye ubora kusaidia maua ya kahawa Kutoka Mengi pia, yasidondoke ovyo.

Mwongozo wa Dawa

Tunakupa ratiba nzima ya kupiga dawa (Spray Program) kudhibiti kimamba na magonjwa ya ukungu.

πŸ“‹ Fomu ya Weka Oda ya Pembejeo na Mbolea

Tumia kitufe cha WhatsApp hapa chini kuwasiliana nasi moja kwa moja au jaza fomu kuagiza Booster Power Jelly na viuatilifu vya kahawa.

Bonyeza Hapa Kuweka Oda WhatsApp
Inatusaidia kukadiria kiasi cha dawa/mbolea unayohitaji.
Ombi Lako la Agizo Limetumwa! πŸŽ‰

Asante kwa kuwasiliana na miche.co.tz! Tutakupigia simu au kukutumia ujumbe wa WhatsApp ndani ya saa 24 kupitia namba uliyoweka. Unaweza pia kututumia ujumbe moja kwa moja kwa WhatsApp: 0765 562 967.

miche.co.tz

Kitalu na kituo kikuu cha pembejeo bora za kilimo kisasa nchini Tanzania. Tunalenga kuongeza tija na mavuno ya wakulima wetu.

Mawasiliano

πŸ“ Njombe, Iringa, Mbozi, Mbeya, Ruvuma)

πŸ“ž 0765 562 967

πŸ’¬ WhatsApp

🌐 miche.co.tz

Β© 2026 miche.co.tz – Haki zote zimehifadhiwa. Kitalu cha Njombe, Tanzania.
TOSCI βœ“Pembejeo βœ“Agribase Bioscience βœ“
Imetumwa!