Ufungaji Mifumo ya Kisasa ya Umwagiliaji na Pump Imara
Tunabuni na kufunga drip irrigation, sprinklers na pump za umwagiliaji zinazookoa maji na kuongeza mavuno shambani kwako.
Huduma za Kisasa za Kilimo Biashara
Tunatoa huduma kamilifu kuanzia upimaji wa udongo na uandaaji wa shamba hadi ufungaji wa umwagiliaji na masoko.
Ufungaji Mifumo ya Umwagiliaji
Usanifu na ufungaji wa mifumo ya matone (drip), sprinkler, na mabomba kwa matumizi sahihi ya maji shambani.
Uzalishaji na Uuzaji Miche
Miche bora ya matunda, mbogamboga na miti iliyothibitishwa ubora na yenye uwezo wa kuzaa kwa haraka.
Layout na Uandaaji wa Mashamba
Upimaji wa mistari, uchimbaji mashimo kwa vipimo vya kitaalamu na mpangilio bora wa shamba la kisasa.
Kupima Udongo (Soil Testing)
Uchunguzi wa afya ya udongo, pH na virutubisho ili kujua zao sahihi na mpango bora wa mbolea.
Ushauri wa Kilimo na Masoko
Mwongozo wa kitaalamu kuanzia kupanda, kudhibiti magonjwa hadi kukuunganisha na masoko ya uhakika.
Uuzaji wa Mashamba / Ardhi
Tunakuwezesha kupata mashamba na ardhi yenye rutuba, maji ya uhakika na nyaraka salama kwa kilimo.
Bidhaa Bora kwa Kilimo Chenye Tija
Chagua miche bora iliyothibitishwa na vifaa vya kisasa vya umwagiliaji kutoka Miche Farm Services.
Miche ya Parachichi
Miche bora ya parachichi (Hass) iliyopandikizwa kitaalamu, isiyo na magonjwa na inayozaa matunda yenye soko kubwa ndani na nje ya nchi.
Miche ya Maembe
Miche ya kisasa ya maembe iliyobebeshwa (grafted) inayoanza kuzaa mapema ndani ya muda mfupi na kustahimili hali mbalimbali za hewa.
Pump za Umwagiliaji
Pump imara za kusukuma maji shambani pamoja na vifaa kamili vya drip na sprinkler kwa mashamba madogo na makubwa.
Mshirika Wako Mwaminifu Katika Kilimo Biashara Tanzania
Miche Farm Services (miche.co.tz) ni kampuni ya kilimo biashara na huduma za kitaalamu za kilimo inayowaunganisha wakulima na miche bora, teknolojia ya umwagiliaji, upimaji udongo na masoko ya uhakika.
Our Vision (Dira Yetu)
Kuwa kituo kikuu na kinachoaminika zaidi cha huduma za kilimo cha kisasa, miche bora na suluhisho za umwagiliaji Afrika Mashariki.
Our Mission (Dhamira Yetu)
Kumwezesha kila mkulima kuongeza uzalishaji na kipato kupitia miche iliyothibitishwa, ushauri wa kitaalamu na teknolojia rahisi.
Timu ya Wataalamu wa Kilimo (SUA)
Kutana na viongozi na wataalamu wetu waliobobea katika Horticulture na Agronomy kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Tazama Video za Mafunzo ya Kilimo na Umwagiliaji
Jifunze hatua kwa hatua jinsi tunavyozalisha miche, kupima udongo, kuandaa mashamba na kufunga mifumo ya umwagiliaji kupitia YouTube playlist yetu rasmi.
Tafuta Mwongozo wa Zao, Miche au Kalenda ya Msimu
Wasiliana na Miche Farm Services
Tuko tayari kukuhudumia kwa ushauri wa kilimo, oda za miche, upimaji udongo na ufungaji wa mifumo ya umwagiliaji.
Official Company Payment Channels
Malipo yote ya miche, vifaa vya umwagiliaji na huduma za shamba yanafanyika kupitia akaunti rasmi ya kampuni na unapewa risiti ya EFD.