Skip to content
KAMANDA 537.5 SE: Kiua Gugu Bora cha Mahindi na Miwa | MICHE.CO.TZ
Kiua Gugu Kinachochagua (Selective Herbicide)

KAMANDA 537.5 SE: Kiboko ya Magugu Kwenye Mahindi na Miwa

KAMANDA ni kiua gugu chenye nguvu kinachodhibiti nyasi na magugu yenye majani mapana kabla na mapema baada ya kuota. Linda mmea wako, ongeza mavuno.

Chupa ya Dawa ya KAMANDA 537.5 SE Herbicide kwa ajili ya Mahindi
Hulinda Mmea Wa Mahindi & Miwa

KAMANDA 537.5 SE Ni Nini?

KAMANDA 537.5 SE ni dawa ya kuua magugu ya kabla ya kuibuka (pre-emergence) na mapema baada ya kuibuka (early post-emergence). Inafanya kazi kwa kuchagua magugu kwa ajili ya kudhibiti magugu ya aina mbalimbali—yale ya majani mapana na yale ya kudumu—katika mashamba ya mahindi, miwa na mahindi matamu bila kudhuru zao kuu.

Viambato (Active Ingredients)

Uwezo mkubwa wa KAMANDA unatokana na mchanganyiko wa nguvu wa viambato vitatu (3) muhimu vinavyofanya kazi kwa ushirikiano:

37.5 g/L Mesotrione
375 g/L S-metolachlor
125 g/L Terbuthylazine

Dosi na Jinsi ya Kutumia

Kipimo cha Kutumia Kiasi cha Dawa Kiasi cha Maji
Kwa Pampu Ndogo (Mkulima Mmoja) 300 ml Lita 20
Kwa Ekari Moja (1 Acre) Lita 1.5 Lita 200 (Pampu 10 za Lita 20)
Kwa Hekta Moja (1 Hectare) Lita 3.0* Kulingana na hitaji (Lita 200+)

*Fuatilia maelekezo ya mtaalamu wetu unaponunua kwa matumizi ya mashamba makubwa sana.

Vifungashio Vinavyopatikana

Tuna saizi tofauti kukidhi mahitaji ya shamba lako, iwe dogo au kubwa.

5 Lita
1 Lita
500 ml

Jifunze Zaidi (YouTube)

Mafunzo ya Kilimo Cha Kisasa
Tembelea YouTube

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Hapana, KAMANDA ni selective herbicide. Inachagua magugu na kuyaangamiza bila kudhuru zao la mahindi, mahindi matamu, wala miwa endapo itatumika kwa dosi sahihi inayopendekezwa.

Wakati mzuri zaidi ni kabla magugu hayajaota sana au magugu yakiwa bado machanga (majani 2 hadi 4). Inaweza kupigwa mara tu baada ya kupanda (pre-emergence) au mahindi yakiwa tayari yameota lakini magugu bado ni madogo (early post-emergence).

Inashauriwa kupiga dawa wakati ambao hakuna dalili za mvua kwa angalau masaa 2 hadi 4 ijayo ili dawa iweze kufyonzwa vizuri na majani ya magugu na kuganda kwenye udongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *