KAMANDA 537.5 SE: Kiboko ya Magugu Kwenye Mahindi na Miwa
KAMANDA ni kiua gugu chenye nguvu kinachodhibiti nyasi na magugu yenye majani mapana kabla na mapema baada ya kuota. Linda mmea wako, ongeza mavuno.
Yaliyomo (Table of Contents)
KAMANDA 537.5 SE Ni Nini?
KAMANDA 537.5 SE ni dawa ya kuua magugu ya kabla ya kuibuka (pre-emergence) na mapema baada ya kuibuka (early post-emergence). Inafanya kazi kwa kuchagua magugu kwa ajili ya kudhibiti magugu ya aina mbalimbali—yale ya majani mapana na yale ya kudumu—katika mashamba ya mahindi, miwa na mahindi matamu bila kudhuru zao kuu.
Viambato (Active Ingredients)
Uwezo mkubwa wa KAMANDA unatokana na mchanganyiko wa nguvu wa viambato vitatu (3) muhimu vinavyofanya kazi kwa ushirikiano:
Dosi na Jinsi ya Kutumia
| Kipimo cha Kutumia | Kiasi cha Dawa | Kiasi cha Maji |
|---|---|---|
| Kwa Pampu Ndogo (Mkulima Mmoja) | 300 ml | Lita 20 |
| Kwa Ekari Moja (1 Acre) | Lita 1.5 | Lita 200 (Pampu 10 za Lita 20) |
| Kwa Hekta Moja (1 Hectare) | Lita 3.0* | Kulingana na hitaji (Lita 200+) |
*Fuatilia maelekezo ya mtaalamu wetu unaponunua kwa matumizi ya mashamba makubwa sana.
Vifungashio Vinavyopatikana
Tuna saizi tofauti kukidhi mahitaji ya shamba lako, iwe dogo au kubwa.
Jifunze Zaidi (YouTube)
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)
Hapana, KAMANDA ni selective herbicide. Inachagua magugu na kuyaangamiza bila kudhuru zao la mahindi, mahindi matamu, wala miwa endapo itatumika kwa dosi sahihi inayopendekezwa.
Wakati mzuri zaidi ni kabla magugu hayajaota sana au magugu yakiwa bado machanga (majani 2 hadi 4). Inaweza kupigwa mara tu baada ya kupanda (pre-emergence) au mahindi yakiwa tayari yameota lakini magugu bado ni madogo (early post-emergence).
Inashauriwa kupiga dawa wakati ambao hakuna dalili za mvua kwa angalau masaa 2 hadi 4 ijayo ili dawa iweze kufyonzwa vizuri na majani ya magugu na kuganda kwenye udongo.

